Mapigano yasita kwa jumla Ukraine
Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani
wamesema wameridhika na namna makubaliano ya kusitisha mapigano
yanavyofuatwa kwa jumla mashariki mwa Ukraine.
Walioshuhudia matukio huko wanasema katika maeneo mengi kuna utulivu, ingawa ni utulivu wa wasiwasi, isipokuwa katika eneo la mji wa Debaltseve ambako wapiganaji wanaoipendelea Urusi wameendelea kuwashambulia wanajeshi wa serikali ambao wamewazingira katika mji huo muhimu kwa usafiri.
Hata katika eneo hilo, mapigano siyo makali kama yalivyokuwa.
Shirika la usalama la Ulaya, OSCE, linasema kuwa wapiganaji wamekataa kuruhusu wachunguzi wa OSCE kuingia katika maeneo yao.
Shirika hilo piya linasema makubaliano ya kusitisha mapigano yanafuatwa.
Hatua ya pili ya kurejesha amani ni kwa pande zote mbili kuondosha silaha nzito kwenye mpaka wa mapigano hapo Jumane.
Mapigano yasita kwa jumla Ukraine
Reviewed by Unknown
on
Februari 15, 2015
Rating:
Hakuna maoni: