Safari ya mwisho ya watoto waliouawa na mwanamke aliyekula mioyo yao Kenya, #RIP
Moja ya taarifa kutoka Nairobi Kenya ambayo ilisikitisha sana ni tukio la watoto watatu kuuawa na mwanamke mmoja ambaye baada ya kuwaua halafu akawapasua na kula mioyo ya watoto hao.
Mwanamke huyo Catherine Muthoni alimuua mtoto wake mmoja mwenye umri wa miaka kumi na baadaye kuua watoto hao wawili wa jirani.
Tukio la leo katika eneo la makaburi ya Lang’ata limewatoa wengi machozi wakikumbuka jinsi watoto hao walivyofariki kwa mateso ambapo familia ya watoto hao wameamua kufanya mazishi ya watoto wote wawili kwenye kaburi moja.
Mwanamke huyo anashikiliwa na Polisi kesi yake ikiendelea ambapo Mahakama iliagiza afanyiwe uchunguzi kama ana matatizo ya akili huku upelelezi wa kesi yake ukiendelea.
Hapa iko taarifa hiyo kwenye video kutoka K24 TV Kenya..
Safari ya mwisho ya watoto waliouawa na mwanamke aliyekula mioyo yao Kenya, #RIP
Reviewed by Unknown
on
Februari 25, 2015
Rating:
Hakuna maoni: