TANGAZO


Ubalozi wa marekani nchini Yemen
Ubalozi wa Uingereza nchini Yemen
Ufaransa imejiunga na Marekani na Uingereza kufunga balozi yake nchini Yemen kutokana na kudorora kwa usalama nchini humo.
Taarifa kutoka Uingereza na Marekani zinasema kuwa wanaondoa oparesheni zao zote za kibalozi kutoka nchini Yemen na kuwataka raia wake kuondoka mara moja.
Wizara ya ulinzi nchini Marekani inasema kuwa kudorora kwa usalama nchini Yemen kumetokana na kuongezeka kwa shughuli za kigaidi na ghasia.
Ubalozi wa Ufaransa mjini Sanaa umesema utafunga shughuli zake kuanzia Ijumaa.
Tangazo hilo linajiri huku waasi wa kishia kutoka kazkazini mwa Yemen wanaojulikana kama Houthi wakiimarisha oparesheni zao za kijeshi baada ya kuuteka mji mkuu wa sanaa.
Uvamizi wa waasi hao katika mji wa sanaa ulisababisha kujiuzlu kwa rais Abd-Rabbu Mansour Hadi ambaye ni mshirika wa Marekani

Reviewed by Unknown on Februari 11, 2015 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.