Waliowajeruhi polisi TZ wasakwa
Polisi nchini Tanzania wamesema wanawasaka watuhumiwa waliowajeruhi askari sita kwa risasi mkoani Tanga.
Askari
hao walijeruhiwa wakati wakifanya kazi ya kuwatafuta watuhumiwa wa
uhalifu wa kutumia silaha wanaodaiwa kuwa walijificha eneo moja nje ya
mji wa Tanga wakiwa na silaha.Awali kulizagaa taarifa na hofu kuwa wahusika walikuwa na itikadi za kigaidi, lakini taarifa ya maandishi iliyotolewa na polisi imewaita watu hao kuwa ni majambazi na kwamba msako wa kuwatafuta unaendelea.
Hata hivyo taarifa haikuleleza wanaotafutwa ni watu wangapi, ingawa imetaja kuhusika kwa jeshi lenye silaha jambo linaloashiria mapambano yalikuwa makali.
Mambo yalivyo kuwa katika mapango ya amboni mkoani Tanga
Waliowajeruhi polisi TZ wasakwa
Reviewed by Unknown
on
Februari 15, 2015
Rating:
Hakuna maoni: