Jana ilikuwa birthday ya Bobbi Kristina, ujumbe wa family na mpenzi wake
Ni zaidi ya mwezi mmoja Bobbi Kristina, mtoto wa marehemu mwanamuziki Whitney Houston amelazwa Hospitali baada ya kukutwa akiwa hana fahamu ndani ya bafu nyumbani kwake Georgia, Marekani ambapo tukio hilo linahusishwa na utumiaji wa dawa za kulevya.
Bado kumekuwa na ripoti za kuvutana kuhusu hali yake kiafya, wapo wanaosema hali ni mbaya sana lakini familia yake mara nyingi imekanusha kuhusu taarifa hizo.
Jana ilikuwa birthday yake kutimiza miaka 22, ndugu wametuma salamu zao kumtakia heri ya kuzaliwa huku wakionesha matumaini yao hali ya kiafya ya Bobbi kuendelea vizuri; “leo ni sherehe ya siku yake ya kuzaliwa, anatimiza miaka 22.. tunaomba muendelee kumkumbuka kwenye maombi ili apone..“
Jana ilikuwa birthday ya Bobbi Kristina, ujumbe wa family na mpenzi wake
Reviewed by Unknown
on
Machi 05, 2015
Rating:
Hakuna maoni: