WATU 45 WAFARIKI MSIKITIN YEMEN
Zaidi ya watu 45 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, baada ya watu wa kujitolea muhanga kujilipua misikitini nchini Yemen.
Watu hao wameuwawa katika milipuko iliyolenga misikiti katika mji mkuu Sanaa wakati wa sala ya Ijumaa.Waandishi Habari wanasema kuwa, misikiti yote miwili ni maeneo ya maombi kwa waislamu wengi ambao aaasi wa Ki-Shia, maarufu kwa jina Houthis, wanaodhibiti mji mkuu wa Sanaa.
Kwa miezi kadhaa sasa, kumeshuhudiwa taharuki kubwa kati ya makundi hasimu nchini Yemen, pamoja na makundi yaliyo na uaminifu na mtandao wa Al-Qaeda yaliyo katika maeneo ya kusini na mashariki mwa taifa hilo.
WATU 45 WAFARIKI MSIKITIN YEMEN
Reviewed by Unknown
on
Machi 20, 2015
Rating:
Hakuna maoni: