Chama cha madereva cha itahadharisha serikali madhara yanayoweza kutokea baada ya ahadi za Mawaziri kushindwa kutatua matatizo yao.
Chama cha madereva wa mabasi kimeitahadharisha serikali juu ya athari zinazoweza kujitokeza baada ya ahadi ya mawaziri wa wizara tatu ya kuzungumza na uongozi wa chama hicho ili kupata suluhisho la kudumu Aprili 18 kushindikana.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini dar es salaam makamu mwenyekiti wa chama hicho Bw.Boniface Prospar amesema hakuna dereva ambaye amepinga agizo la serikali lililowataka kwenda kusoma isipokuwa wanachohitaji ni madai yao ya msingi ya muda mrefu yashughulikiwe kwanza ikiwemo mikataba ya ajira ambayo itawawezesha kuwa na uhakika na wanachokwenda kusoma pamoja na bima itakayowasaidia pindi wanapopata matatizo.
Wakizungumzia suala la ajali baadhi ya madereva wa mabasi wametupia lawama kwa wamiliki wa mabasi hayo kwa madai kuwa ndiyo chanzo kikubwa kwani wanawaagiza kutembea zaidi ya kilomita 80 kwa saa zilizoagizwa na serikali na dereva anapofanya kinyume ananyang'anywa gari huku wakilalamikia tatizo la miundombinu mibovu.
Akijibu lawama hizo katibu mkuu wa chama cha wamiliki wa mabasi TABOA Bw. Enea Mrutu amesema TABOA imeunda kamati ya watu wanne inayojulikana kwa jina la usalama na maadili ambayo itachunguza suala la ulevi kwa madereva,kuzingatia muda,utekelezaji wa agizo la serikali la kuwa na madereva wawili kwa safari ndefu, miundombinu,wamiliki ili kubaini kiini cha malalamiko yao pamoja na Polisi.
Chama cha madereva cha itahadharisha serikali madhara yanayoweza kutokea baada ya ahadi za Mawaziri kushindwa kutatua matatizo yao.
Reviewed by Unknown
on
Aprili 25, 2015
Rating:
Hakuna maoni: