TANGAZO

CUBA YAONDOLEWA KATIKA ORODHA YA KUFADHILI UGAIDI


Rais wa Marekani Barack Obama ( kulia ) akisalimana na Rais wa Cuba, Raul Castro. 

Ikulu ya Marekani imesema Rais Barack Obama ameiondoa nchi ya Cuba katika orodha ya mataifa ambayo yanafadhili ugaidi, ikiwa ni moja ya hatua muhimu ya kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. 

Cuba iliorodheshwa kuwa moja kati ya mataifa yanayofadhili ugaidi March 01' 1982, ikiwa ni pamoja na nchi za Iran mwaka 1984, Sudan 1993 na Syria iliyowekwa katika orodha ya kufadhili ugaidi mwaka 1979. 

Serikali ya Cuba imepokea kwa mikono miwili uamuzi huo wa Rais Obama, lakini imesisitiza kuwa tangu mwanzo nchi hiyo haikustahili kuwekwa katika orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi kwani haikuwahi kufanya hivyo.
CUBA YAONDOLEWA KATIKA ORODHA YA KUFADHILI UGAIDI CUBA YAONDOLEWA KATIKA ORODHA YA KUFADHILI UGAIDI Reviewed by Unknown on Aprili 15, 2015 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.