Bado naishi na risasi mwilini : Tundu Lissu
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu ameeleza kuwa kwa saa hali yake
imeimarika sana huku akiendelea na mazoezi ya viungo kutokana na kujeruhiwa sehemu kubwa ya mwili wake.
“Hali yangu ya Afya abado inaendelea vizuri,Bado niko Hospitali mguu wangu unauona uko juu maana yake ni kwamba sijapona kabisa, nimevaa nguo za hospitali maana yake bado ni mgonjwa. Lakini niwaambie watanzania pamoja na wananchi wengine wote ambao wamefuatilia afya yangu tangu tarehe 7 septemba, kwamba naendelea vizuri sana,” alisema Tundu Lissu.
Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, nyumbani kwake eneo la Area D, Dodoma, ameeleza kuwa kwa sasa hana jeraha lolote la risasi na hali yake ni nzuri kuliko awali huku akitaja kuwa bado ana risasi moja ndani ya mwili wake ambayo haijatolewa.
“Hivi tunavyozungumza sina jeraha lolote la risasi. Risasi 16 ziliingia kwenye mwili wangu na 7 zilitolewa na madaktari hapahapa, na moja bado iko kwenye mwili wangu. Lakini sina majeraha yoyote ya risasi. Hali ni nzuri kuliko nilivyoletwa, nililetwa vipande vipande kabisa,” alisema Lissu.
Akizungumzia vuguvugu za kisiasa zinazoendelea nchini kwa sasa ikiwamo kuhama hama kwa baadhi ya wanachama wanaojitoa katika vyama vyao na kuhamia vingine, Lissu alisema kuwa hilo halitishii kwa namna yoyote ile uhai wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwani wapo watu wengi sana ambao wamehama chama hicho na bado kinaendelea na harakati za kiukombozi.
“Mbunge wa kwanza kabisa wa CHADEMA katika historia ya vyama vingi ya nchi yetu anaitwa Amal WAlim Kabur, ndiye alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa CHADEMA, na mimi nilipojiunga miaka 14 iliyopita, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na mbunge wa CHADEMA Kigoma Mjini, alihamia CCM baada ya kuhamia CCM CHADEMA ilikufa?… Mzee Said Arth Mbunge wa Mpanda Mjini, alirudi CCM, CHADEMA ilikufa?, Dk Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa vipindi vitatu mfululizo, baada ya safari kuwa ndefu mno, akashukia njiani, CHADEMA imekufa?…” alihoji Lissu.
Mbunge Tundu Lissu alieleza pia kuwa kukaa kitandani ndani ya Hospitali kwa muda wa miezi mitatu sasa kunamfanya ‘aimiss’ kazi yake ya Ubunge, kwani ndiyo kazi anayoipendelea zaidi.
“Mimi napenda Ubunge, yale mapambano ya mule ndani, mapambano ya kiitikadi, kisiasa. Unamkaba Waziri Mpaka anakosa pa kukimbilia. Hiyo ndiyo kazi ninayopenda mimi. Na kwa hiyo hakuna kazi ninayoimiss mii kama kazi ya Ubunge Bungeni..” alisema.
Bado naishi na risasi mwilini : Tundu Lissu
Reviewed by Unknown
on
Desemba 22, 2017
Rating:
Hakuna maoni: