Nape Nnauye Avutiwa ANC Ya Afrika Kusinii Ilivyopata Mwenyekiti Wake, Atupa Jiwe Gizani
Mbunge Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni kwa kuhoji vyama vya siasa na wanasiasa Tanzania wanajifunza nini kufuatia mchakato wa uchaguzi ndani ya chama tawala cha (ANC) uliofanyika Afrika Kusini mwanzoni mwa wiki hii kumpata kiongozi wa chama hicho.
Chama
tawala cha African National Congress (ANC) kilikuwa na uchaguzi wa
ndani kumtafuta kiongozi wa juu ya chama hicho ambapo kulikuwa na zoezi
la uchaguzi na nafasi hiyo kugombewa na wananchama wa chama hicho na
kupigiwa kura, ambapo mwisho wa siku Cyril Ramaphosa aliibuka mshindi
kwa kura nyingi zaidi dhidi ya Nkosazana Dlamini-Zuma hivyo Cyril
Ramaphosa kutangazwa Rais wa (ANC).
"Tunajifunza nini kwa mchakato uliopelekea kupatikana kwa Cryll Ramaphosa kama Mwenyekiti wa ANC!? Alihoji Nape Nnauye
Uchaguzi
wa Chama tawala nchini Afrika Kusini (ANC) ulitofautiana na uchaguzi wa
Chama Tawala nchini Tanzania ambapo Mwenyekiti wake alipatikana kwa
kupigiwa kura ya Ndiyo au Hapana wakati Afrika Kusini nafasi hiyo
iligombewa na mtu zaidi ya mmoja.
Nape Nnauye Avutiwa ANC Ya Afrika Kusinii Ilivyopata Mwenyekiti Wake, Atupa Jiwe Gizani
Reviewed by Unknown
on
Desemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni: