Kutoka Mamlaka Ya Mapato TRA
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya mabadiliko ya ulipaji kodi kwa
wafanyabiashara wadogo ambao watalipa robo ya kwanza ya malipo ndani ya
siku 90 badala ya njia ya awali ya kufanyiwa makadirio.
Mabadiliko
hayo yatawasaidia wafanyabiashara kuanzia waliposajiliwa tofauti na
utaratibu uliokuwepo wa kulipia kodi hiyo hata kabla mfanyabiashara
hajaanza kufanya biashara.
Hayo
yameelezwa leo Januari 2 na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah
Mwandumbya wakati wa kuzindua kampeni ya usajili wa walipa kodi ambapo
amesema wanatarajia kusajili walipakodi wapya milioni moja kwa mwaka
2017/2018.
Mwandumbya
amesema TRA hawana wakala yeyote aliyepewa jukumu la kusajili au hata
kutoa fomu ya usajili hivyo amewataka wananchi wajihadhari na vishoka
ambao watatumia mwanya na kuharibu kampeni hiyo.
"Hatuna
mtu yeyote hivyo ni wazi kupitia vyombo vya habari wananchi wanatakiwa
kuwa makini kwani usajili utafanyika katika ofisi za TRA na katika vituo
maalumu," amesema Mwandumbya.
Amesema kampeni hiyo na mabadiliko hayo yamekuja kwa nia ya kuongeza hamasa kwa wananchi ili wawe na utaratibu wa kulipa kodi.
Mwandumbya ameendelea kusisitiza azma ya serikali kukusanya kodi na kukuza uchumi wa viwanda na kuleta maendeleo kwa Taifa.
Kutoka Mamlaka Ya Mapato TRA
Reviewed by Unknown
on
Januari 02, 2018
Rating:
Hakuna maoni: