Waziri Jafo: Madarasa Ya Nyasi, Tembe, Udongo Yasitumike Katika Shule Zote Nchini
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye
maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama
yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja
kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora.
Waziri
Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi
kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa
viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi.
“Viongozi
wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo
mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka leo
wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana madarasa bora watoto
wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa Nyasi nahitaji
muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe
yotoweke kabisa; Mjenge madarasa ambayo wanafunzi watajiskia fahari
kusoma”Alisema Waziri Jafo.
Waziri
Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa
Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo
yote yote Nchini.
Niwapongeze
baadhi ya Wakurugenzi ambao mpaka sasa wamefanya kazi nzuri sana ya
Usimamizi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Afya wameshakamilisha ujenzi
na wamejenga mpaka Njia za kutembelea(Walk Way) katika vituo hivyo na
nataka mpaka Tarehe 30 April 2018 Kila Halmashauri iliyopokea Fedha za
ujenzi wa Miundombinu ya Afya iwe imekamilika.
Waziri
Jafo alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo
mafunzo haya kuheshimu mipaka yao ya kazi, kuboresha mahusiano kazini,
kutunza Siri za Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.
Awali
akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja amesema kuwa mafunzo haya
yanakamilisha mtiririko wa mafunzo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa K. Majaliwa miezi nane
iliyopita na baada ya mafunzo haya yanayoanza leo tutakuwa tumewafikia
Viongozi 324.
Prof.Semboja
aliongeza kuwa Lengo la mafunzo haya ni yale yale ambayo ambayo
yamelengwa tangu Kikao cha Mwanzo cha Mafunzo haya ambayo ni kuimarisha
uwezo wa kufanya maamuzi wa Kimkakati kwa kuzingatia mahitaji ya jamii
kwa manufaa mapana ya sasa nay a baade ya Jamii Tunayoihudumia.
Sambamba
na hilo Mkutano huu pia unalenga kuongeza uwezo wa Viongozi wetu katika
kuongoza watu na rasillimali zingine zilizoko kwenye maeneo yetu ili
kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya pamoja.
Alisisitiza
kuwa Mafunzo haya yatajielekeza katika Kuimarisha Sifa Binafsi za
Viongozi kwa sababu Viongozi ndio wanaowasimamia wananchi katika kiLA
Eneo hivyo ni lazima kila kiongozi aweze kujitenegenezea Sifa binafsi
ili akubalike na kuhesimika katika Jamii husika.
“Sifa
hizi binafsi tunazozizungumzia ni Ushawishi, Kuaminika, Uadilifu,
Mtenda Haki, Muumini wa Utawala bora na Utawala wa Sheria na zaidi kuwa
mchahapa kazi na awe na weledi wa hali ya juu sasa haya yote
yatafundishwa kupitia mafunzo haya ya namna gani Kiongozi anaweza
Kujijengea Sifa Binafsi katika Jamii tunazoziongoza.
Akitoa
Neno la Shukrani kwa niaba ya viongozi walioshiriki katika Mafunzo haya
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti ameshukuru OR-TAMISEMI
na Taasisi ya Uongozi kwa kuandaa mafunzo haya na zaidi ameahidi Umakini
wa washiriki kwa siku zote za mafunzo.
Mafunzo
haya ya awamu ya Nne na ya mwisho kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa
Mamlaka za Serikali za Mitaa imegususa Viongozi kutoka katika Mikoa ya
Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
Waziri Jafo: Madarasa Ya Nyasi, Tembe, Udongo Yasitumike Katika Shule Zote Nchini
Reviewed by Unknown
on
Januari 29, 2018
Rating:
Hakuna maoni: