Upatikanaji wa dawa waongezeka na kufikia asilimia 95
Serikali yasema upatikanaji wa dawa katika hospitali, zahanati na vituo vya afya vya hospitali umefikia asilimia 95 kutoka ilivyokuwa awali 80% huku ikibainisha kuwa bei ya dawa kushuka kwa 40%.
Serikali imesema utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya juu ya Tazara Fly Over umefikia asilimia 70 ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
Serikali imesema kuanzia mwezi Juni au Julai mwaka huu itaanza ujenzi wa barabara za juu (FlyOver) kwenye makutano ya barabara za Chang’ombe, Uhasibu, Kamata, Morocco, Mwenge, Magomeni na Tabata, ujenzi huo utasaidia kuondoa changamoto ya foleni jijini Dar es Salaam.
Awamu ya pili ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuanza mwaka huu, mradi huo utahusisha ujenzi wa barabara za mwendokasi za Kilwa hadi Mbagala, na Uhuru hadi Gongo la Mboto.
Serikali imepanga kubadilisha mfumo wa masoko ya mazao mbalimbali kwa kuanzisha Soko la Kimataifa la Bidhaa za Kilimo.
Upatikanaji wa dawa waongezeka na kufikia asilimia 95
Reviewed by Unknown
on
Februari 07, 2018
Rating:
Hakuna maoni: