TANGAZO

Jamii ya Wamakonde kupewa uraia Kenya


 
 
Maelfu ya watu wa jamii ya Wamakonde wanapewa uraia wa Kenya kwa mara ya kwanza.
Kabila la Makonde linaloishi pwani ya Kenya walihama kutoka Msumbiji enzi za ukoloni kuja Kenya na kufanya kazi katika mashamba ya miwa.

Watakaposajiliwa, Jamii hiyo ya Wamakonde elfu tatu watapewa vitambulisho na kuwa kabila la 43 nchini Kenya.
Kushindwa kwao kujitambulisha kunamaanisha kwamba kwa miongo kadhaa wameshindwa kujisajili katika shule ama hata kutafuta kazi.
Jamii ya Wamakonde kupewa uraia Kenya Jamii ya Wamakonde kupewa uraia Kenya Reviewed by Unknown on Februari 13, 2015 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.