TANGAZO

Al Azhar yawafuta kazi wafuasi wa Ikhwanul Muslimin




Al Azhar yawafuta kazi wafuasi wa Ikhwanul Muslimin
Vyombo vya habari nchini Misri vimeripoti kwamba, tangu kulipoanza muhula mpya wa masomo nchini humo, zaidi ya wajumbe 80 wa baraza la elimu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar wamefutwa kazi.

 Duru za habari zimemnukuu Hussein Uweidha, Mkuu wa Ofisi Kuu ya Walimu katika chuo hicho akisema kuwa, mbali na shakhsia hao 80, walimu wengine 100 wamepelekwa idara ya uchunguzi inayoshughulikia maadili kwa ajili ya kusailiwa zaidi. Ameongeza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kwamba asilimia 70 ya viongozi wa hivi sasa wa Chuo Kikuu cha al-Azhar wana mafungamano na Harakati ya Ikhwanul Muslimin iliyopigwa marufuku nchini Misri. Amedai kuwa, uwepo wa shakhsia hao katika chuo hicho, umekuwa ukiwachochea wanafunzi kufanya jinai na uharibifu katika idara za serikali, na hivyo kukiongoza chuo hicho cha kihistoria kuelekea kwenye mustakbali usio na mwanga.
Al Azhar yawafuta kazi wafuasi wa Ikhwanul Muslimin Al Azhar yawafuta kazi wafuasi wa Ikhwanul Muslimin Reviewed by Unknown on Februari 14, 2015 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.