KITISHO KUWEPO KWA ALSHABAAB TANGA
SEKESEKE cha kitisho cha kuwepo kwa kikundi cha kihalifu cha Al Shaaab Tanga, kimeishtua Tanga na wananchi hasa wanaoishi eneo la Amboni na baadhi ya familia zenye makazi yake kuhama.
Wakizungumza na kumekucha blog wakazi wa eneo hilo wamesema hadi muda huo hawana uhakika wa kuwepo kwa kikundi cha Alshabab au kama ni Majambazi na hivyo kusikiliza taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi.
Wamedai kusikia milio ya risasi na bunduki kwa takribani kuanzia saa 8 usiku hadi asubuhi na walipoamka habari za watu ni kuwepo kwa Alshabab ila wanasema hakuna uhakika wa jambo hilo.
Kamanda wa Operesheni Taifa, Paul Chagonja anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari saa 9 mchana huu Ofisi za kamanda wa Polisi Tanga.
Fuatilia blog ili kujua nini hasa kimejiri na ukweli wa jambo hili kupitia amribinramadhani blogsport.com
KITISHO KUWEPO KWA ALSHABAAB TANGA
Reviewed by Unknown
on
Februari 14, 2015
Rating:
Hakuna maoni: