Mapambano Makali Bado Yanaendelea Kuwasaka MAGAIDI wa Tanga.
Kutokana na wahalifu wanaopambana na polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutokamatwa, hali ya wasiwasi imeendelea miongoni mwa wakazi wa mjini hapa.
Sasa
wananchi hao wameiomba Polisi kutoa tamko, kuhusu kikundi
kilichorushiana risasi na askari Polisi na kusababisha kifo cha
mwanajeshi mmoja.
Aidha,
wananchi hao wameitaka Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu mwendelezo wa
matukio mengi ya uhalifu wa kutumia silaha, ambayo bado hayajapatiwa
ufumbuzi, ikiwemo kutokamatwa kwa watuhumiwa wa matukio hayo.
Hata
hivyo, Msemaji wa Polisi, Advera, alisema Jeshi lake halina taarifa
zaidi ya iliyotolewa juzi na Mkuu wa Opersheni wa jeshi hilo, Kamishna
Paul Chagonja.
Habari
za kipolisi zinasema kwamba bado wanaendelea kusaka wahalifu hao huku
baadhi ya vikosi vya ulinzi na usalama, vimeongezwa kwa ajili ya
kupambana na wahalifu hao.
Juzi
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi walipambana na kundi la
wahalifu katika maeneo ya mapango ya Amboni na kusababisha wanajeshi
wanne na polisi wawili kujeruhiwa. Hata hivyo, kuna habari kuwa majeruhi
mmoja ambaye ni mwanajeshi alifariki baadaye akiwa hospitalini.
Habari zingine zinasema kwamba majeruhi wengine ambao ni polisi wanne na mwanajeshi mmoja, wanaendelea vizuri.
Kuhusu mwanajeshi aliyekufa, polisi wamegoma kuzungumzia suala hilo, lakini habari zinasema aliyekufa ni mwanajeshi mwenye cheo cha sajenti.
Kuhusu mwanajeshi aliyekufa, polisi wamegoma kuzungumzia suala hilo, lakini habari zinasema aliyekufa ni mwanajeshi mwenye cheo cha sajenti.
Wananchi
wametoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana, walipozungumzia tukio la
juzi, lililosababisha mapigano ya kurushiana risasi baina ya askari na
wahalifu, wanaodaiwa kuficha silaha katika eneo la Mapango ya Amboni,
nje kidogo ya mji wa Tanga.
Walisema
mpaka sasa bado hawajaridhishwa na mwenendo wa utendaji wa Jeshi la
Polisi mkoani hapa, pamoja na taarifa hafifu wanazotoa, kuhusu namna
walivyoshughulikia tukio hilo la juzi kwenye mapango hayo ya Amboni.
Ibrahim
Mshote, mkazi wa Ngamiani Kati, alisema mbali na tukio la juzi, yapo
matukio mengine yakiwamo yaliyosababisha mauaji kwa raia, ambao
walivamiwa na kuporwa mali na watuhumiwa kushindwa kupatikana.
Alisema hakuna taarifa za mwendelezo wa kushughulikiwa kwa matukio hayo.
Alisema hakuna taarifa za mwendelezo wa kushughulikiwa kwa matukio hayo.
“Kwa
mfano kuna wananchi walilipuliwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati
wakitazama mpira kwenye kibanda cha video hapo Amboni… pia yupo
mfanyabiashara wa eneo la Mkumbara wilayani Korogwe ambaye hivi karibuni
alivamiwa na kuuawa kwa risasi kabla ya kuporwa mali, pia tukio la
utekaji wa gari eneo la Michungwani wilayani Handeni baada ya kuwekewa
magogo barabarani”, alisema.
Aliongeza
“Katika matukio kama hayo, tunaambiwa tu wahalifu hawakupatikana,
upelelezi unaendelea, lakini ni zaidi ya wiki mbili sasa hakuna taarifa
zozote zinazoonesha juhudi za mwendelezo wa kudhibiti wahalifu kama hao,
badala yake matukio yameendelea kuongezeka”.
Miriam
Jonas, mkazi wa Barabara ya Tano jijini Tanga, alisema kitendo cha
askari kunyang’anywa silaha mbili za SMG zenye risasi 60 kwenye kibanda
cha chipsi ni fedheha kwa kuwa vitendo hivyo vilishasahaulika mkoani
hapa.
“Tulitarajia
wahusika wangekamatwa ndani ya muda mfupi, lakini wapi, Polisi hapa
Tanga imeshindwa kabisa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo hadi Kamishna
Chagonja alipokuja na kuzungumzia tukio la juzi”, alisema.
Aidha,
Mrisho Mashaka mkazi wa Kwaminchi alisema licha ya Chagonja kuwataka
wakazi wa jiji la Tanga kutulia, kwakuwa hali ya usalama imeimarishwa,
bado baadhi ya wananchi wanayo shaka na hofu kubwa kuhusu tamko hilo.
“Kinachoendelea
kutupa hofu ni mgongano wa kauli za polisi kama tulivyosikia kwenye
vyombo vya habari kwamba waliarifiwa kwamba silaha za moto zikiwemo
walizoporwa askari Januari 26 zimefichwa ndani ya mapango, lakini
kilichokutwa ni silaha za jadi yakiwemo mapanga, pinde na mishale na
vifaa vya kutengeneza milipuko”, alidai.
Alisema
vifaa vilivyotajwa kukutwa kwenye eneo la tukio ni tofauti na madhara
waliyopata askari, waliokuwa kwenye operesheni hiyo ya kusaka silaha
hizo, ambayo yamesababisha kifo na majeraha makubwa kwa baadhi yao,
ambao sasa wamelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa ya Bombo.
“Binafsi
bado napata kigugumizi kuelewa taarifa hii kwasababu bado inayo maswali
mengi ya kujiuliza, je hao ni watu wa namna gani ambao wamefanikiwa
kujeruhi vibaya askari na kisha kutoroka na silaha zilizokuwa
zikitafutwa, wameelekea wapi? Je sisi tuko salama?”,alihoji.
Walidai
vipo viashiria vinavyoonesha kwamba hali ya ulinzi na usalama mkoani
hapa, haijatengemaa kutokana na hali ya mazingira iliyobainisha kwamba
wahalifu hao waliweka makazi ndani ya mapango hayo bila kubainika
mapema.
Mbali
ya silaha za jadi, vitu vingine vilivyokutwa ndani ya mapango hayo ni
pikipiki mbili, baiskeli tatu, mavazi ya aina mbalimbali na vyakula,
ambavyo ni dhahiri vinaashiria kwamba watu hao walikuwa wakijipenyeza
ndani ya jamii kutafuta huduma muhimu bila kufahamika kwamba ni
wahalifu.
Aidha,
walisema ripoti ya hivi karibuni ya hali ya uhalifu mkoani Tanga,
ambayo ilitolewa na Kamanda mwishoni mwa mwaka jana ilibainisha
kuongezeka kwa makosa ya uhalifu, yanayofanywa dhidi ya binadamu kwa
asilimia 2.11, ikilinganishwa na takwimu za makosa kama hayo
yaliyoripotiwa mwaka 2013.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai alibainisha hayo wakati akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya ulinzi na usalama mkoani
humo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana.
Kamanda
alisema kwamba mwaka 2014, makosa 7, 970 ndiyo yaliripotiwa kwenye
vituo mbalimbali vya Polisi wilayani, ikilinganishwa na makosa 7,805
yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2013.
Wakazi
hao wa Tanga walidai wanaamini kwamba takwimu hizo ni kiashiria tosha
kwamba mambo hayako sawa, licha ya Kamishna Chagonja kujitahidi kutoa
matumaini.
Kutokana
na mambo kama hayo, walisema kuna umuhimu mkubwa kwa jeshi hilo
kujipanga kimkakati ili kuondoa tatizo hilo haraka kwasababu kila siku
matukio mapya yanaibuka na watuhumiwa hawapatikani.
Hapo chini nimekuwekea Video nyingine ya Magaidi wa Tanga Wakijigamba kupora Silaha:
Hapo chini nimekuwekea Video nyingine ya Magaidi wa Tanga Wakijigamba kupora Silaha:
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
Mapambano Makali Bado Yanaendelea Kuwasaka MAGAIDI wa Tanga.
Reviewed by Unknown
on
Februari 15, 2015
Rating: