Picha na taarifa ya mtu wa Nicki Minaj aliyeuwawa kwa visu, huyu mwingine kachomwa pia.
Hawa jamaa wawili wanaoonekana kwenye picha walikua ni sehemu ya timu ya Nicki Minaj, walikwenda sehemu inaitwa Philadelphia Marekani ambapo ni siku mbili tu zimepita toka waingie kwenye mji huo kwa ajili kujiandaa na ziara ya kimuziki ya Nicki Minaj.
Polisi wamesema aliyefariki ni De’Von Pickett, 29, au Day Day anaeonekana kushoto kwenye picha Eric Parker, 27 mwingine aliyejeruhiwa anaendelea vizuri na matibabu.
Kilichotokea ni wao kuchomwa visu kwenye ugomvi uliotokea wakiwa Baa usiku wa Jumanne na rafiki zao ambapo baada ya kuchomwa visu walikimbizwa Hospitali lakini muda mfupi baadae Day Day akawa amefariki.
Picha na taarifa ya mtu wa Nicki Minaj aliyeuwawa kwa visu, huyu mwingine kachomwa pia.
Reviewed by Unknown
on
Februari 20, 2015
Rating:
Hakuna maoni: