Utaliana yafunga Ubalozi Libya
Ubalozi wa Utaliana mjini Tripoli, Libya, umefungwa na wafanyakazi wake kurejeshwa nyumbani kwa sababu za usalama.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje mjini Rome imesema hoteli ambamo wafanyakazi hao wa ubalozi wakiishi, siyo salama tena.Utaliana ndiyo nchi pekee ya Ulaya iliyokuwa imebaki na ubalozi mjini Tripoli, lakini kuna wasiwasi kuwa wapiganaji Waislamu wa siasa kali watailenga ofisi hiyo.
Mapambano baina ya jeshi la serikali na wapiganaji Waislamu yamekuwa yakiendelea tangu Kanali Gaddafi kupinduliwa; na waziri wa ulinzi wa Utaliana, Roberta Pinotti, amesema nchi yake iko tayari kushiriki kwenye hatua za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao.
Utaliana yafunga Ubalozi Libya
Reviewed by Unknown
on
Februari 15, 2015
Rating:
Hakuna maoni: