TANGAZO

Odinga: Vita dhidi ya ufisadi ni mchezo wa kisiasa


 http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/8a0e224398f445a45b9c0c14f9e82483_XL.jpg
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, amesema kuwa vita dhidi ya ufisadi vinavyoendelea nchini humo si vya dhati na kwamba lengo kuu la serikali ni kuwahadaa wananchi.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu Bw. Odinga amesema hana imani na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) ambayo amesema yenyewe ina matatizo ya ndani na haizungumzi kwa sauti moja

. Raila Odinga ambaye ndiye kinara wa muungano mkuu wa upinzani wa CORD amesema wabunge wa muungano huo watashinikiza serikali iwafuatilie mafisadi halisi badala ya kuwanyooshea vidole watu ambao hawajasailiwa na vyombo vyovyote vya usalama wala tume ya EACC. "Kutaja majina ya watu na kisha kuwashinikiza wajiuzulu kwa muda ili uchunguzi ufanyike dhidi yao si vita vya dhati dhidi ya ufisadi. Kuna haja ya uchunguzi wa kweli kufanywa na wale watakaopatikana na hatia wachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutwa kazi kabisa na kupandishwa kizimbani", amesema mkuu huyo wa upinzani.
Rais Uhuru Kenyatta amewataka maafisa wa serikali waliotajwa kwenye ripoti ya ufisadi ya EACC wajiuzulu kwa muda ili kupisha uchunguzi huru dhidi yao. Tayari mawaziri 5 wametangaza kujiuzulu kwa muda kufuatia agizo hilo la serikali baada ya kubainika kuwa majina yao yako kwenye ripoti hiyo.
Sikiliza mahojiano kamili ya Redio Tehran na Bwana Odinga katika sehemu ya mahojiano ya mtandao huu.
Odinga: Vita dhidi ya ufisadi ni mchezo wa kisiasa Odinga: Vita dhidi ya ufisadi ni mchezo wa kisiasa Reviewed by Unknown on Machi 31, 2015 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.