TANGAZO

FAIDA ZA BINZARI NYEMBAMBA MWILINI



Unapozungumzia binzari nyembamba hiki ni kiungo kinachotumika sana na watu wa pwani ya Afrika Mashariki, Wahindi, Waarabu pamoja na Wachina.


Kiungo hiki asili yake kabisa ni Misria, Uturuki na Mashariki mwa Mediterranean, licha ya kuwa kwa sasa binzari hiyo inaelezwa kutumika sana Kusini Mashariki ya Ulaya, nchi za Kaskazini ya Afrika pamoja China na India.

Mtaalam wa tiba asilia hapa nchini kutoka Mandai Herbalist Clinic, Dk Abdallah Mandai anasema kuwa, binzari nyembamba ndani yake ina nyuzinyuzi, mafuta, protini, calcium, chuma, potassiumphosphorusthismine(vitamin B) riboflavin (vitamin B2) pamoja na vitamin A.

Aidha, mtaalam huyo anabainisha kuwa, mbegu za kiungo hicho hutengenezewa mafuta, ambayo hutumika kutibu minyoo ‘hook worm’ na kusaidia kuhamasisha utokaji wa haja ndogo (mkojo), sambamba na kuondoa gesi tumboni.



Pia mbegu zake zinapotumika vizuri husaidia kutibu wale wenye shida ya kuharisha na kusaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni.

Mbali na hayo kiungo hicho husaidia kuzuia kichefuchefu, lakini pia katika mapishi kiungo hiki husaidia kuongeza radha , mfano kwenye supu, mikate, keki nk.
FAIDA ZA BINZARI NYEMBAMBA MWILINI FAIDA ZA BINZARI NYEMBAMBA MWILINI Reviewed by Unknown on Aprili 13, 2015 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.