MZEE YUSUF KUACHIA MPYA DAR LIVE
MFALME Mzee Yusuf amerudi tena ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar ambapo Aprili 25, mwaka huu anatarajia kuachia ngoma mpya.
Akizungumza na Over The Weekend, Mzee Yusuf anayebamba kunako miondoko ya Taarab alisema kuwa anawashukuru mashabiki kwa kuweza kumudu kwenye muziki kwa muda mrefu na zawadi kubwa atakayoitoa siku hiyo ni wimbo mpya uitwao Kaning’ang’ania Ng’ang’anu.
“Nitakuwa na kundi langu la Jahazi tukiwapa raha za Pwani, nitapiga nyimbo zangu zote tangu natoka na Bendi ya Zanzibar hadi hapa nilipo Jahazi,” alisema Mzee Yusuf
MZEE YUSUF KUACHIA MPYA DAR LIVE
Reviewed by Unknown
on
Aprili 13, 2015
Rating:
Hakuna maoni: