TANGAZO

YANGA INAVYOJIWINDA DHIDI YA WAARABU WA TUNISIA

Kocha Pluijm (mwenye fulana ya njano) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Wachezaji wakijiandaa kupiga mashuti.
Kocha Pluijm akimuangalia Haruna Niyonzima anavyofuata maelekezo aliyompa.

Mashabiki wakifuatilia mazoezi hayo kwenye nyavu
Mchezaji majeruhi, Salum Telela, akifanya mazoezi kuonyesha kuwa anaendelea vizuri
Shabiki huyu alikuwa akiwatolea maneno ya ‘shombo’ wachezaji waliokuwa wakikose ambapo haikujulikana mara moja kama kweli ni shabiki wa Yanga au la
Wachezaji wakiwania mpira
KIKOSI cha timu ya Yanga leo kiliendelea kujifua katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiwinda na mechi yao ya Klabu Bingwa Afrika inayotarajiwa kupigwa Jumamosi ijayo dhidi ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Katika mazoezi hayo kocha mkuu wa kikosi hicho, Hans Der Pluijm, alianza na kuwafundisha wachezaji hao jinsi ya kupiga mashuti makali wawapo karibu na lango la adui. Sambamba na kupiga mashuti ya kumpoteza kipa wa timu pinzani, kocha huyo aliwafundisha wachezaji hao jinsi ya kuwahadaa mabeki wa timu pinzani.
Katika mazoezi hayo mshambuliaji tishio kwa magoli ya vichwa, Mrundi Hamisi Tambwe aliendelea kuwafurahisha mashabiki waliohudhuria  mazoezi hayo kwa kupiga mabao safi kwa kutumia kichwa chake.
YANGA INAVYOJIWINDA DHIDI YA WAARABU WA TUNISIA YANGA INAVYOJIWINDA DHIDI YA WAARABU WA TUNISIA Reviewed by Unknown on Aprili 15, 2015 Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.