MAGUFULI AUNDA TIMU KUFUATILIA MALI ZA CCM
Mwenyekiti
wa CCM, Rais John Magufuli ameunda tume ya watu tisa kufuatilia mali
za chama hicho, akiifananisha na tume aliyoiunda kuchunguza biashara ya
madini nchini.
Miongoni mwa wajumbe wa tume hiyo
itakayoongozwa na Dk Bashiru Ali Kakurwa, ni kada mpya wa chama hicho,
Albert Msando aliyejiunga na CCM Novemba 21 akitokea ACT-Wazalendo.
Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo
Jumatano Desemba 20,2017 mjini Dodoma katika kikao cha kwanza cha
Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichojadili mikakati ya
kuimarisha kazi za CCM na Serikali.
Wajumbe wengine wa tume hiyo ni Walter
Msigwa, Galala Wabanhu, Albert Chalamila, William Sarakikya, Komanya
Kitwara, Dk Fenela Mukangara na Mariam Mangula.
"Nataka nitoe wito na Waziri Mkuu yuko
hapa, hii timu itachunguza mtu yeyote awe wa Serikali au kwenye chama
ili mali zote ziorodheshwe," amesema katika taarifa zilizotolewa na
chama hicho.
"Hii ni tume yangu, ni kama ya makinikia
ila haya ni makinikia ndani ya CCM. Nataka siku moja chama hiki kiweze
kujitegemea," amesema.
Mwenyekiti huyo wa CCM amewataka
Watanzania wanaoshikilia mali za chama hicho kujitokeza na kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa masilahi ya CCM.
MAGUFULI AUNDA TIMU KUFUATILIA MALI ZA CCM
Reviewed by Unknown
on
Desemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni: