WATANZANIA 900,000 WANATUMIA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA UKIMWI
Watoto 10,000 wanaozaliwa Tanzania wana maambukizo ya Ukimwi huku
Watanzania 900,000 wakiendelea kutumia dawa za kufubaza makali ya
ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akifungua majengo ya chuo cha uuguzi cha Mirembe mjini Dodoma.
Waziri Mwalimu amesema kiwango hicho ni kikubwa ambacho kinapaswa
kupunguzwa kwa juhudi za haraka kwani lengo lake ni kuona watoto wote
wanazaliwa bila maambukizo.
Wakati huo Mwalimu amekiri kuwa kiwango cha fedha zinazotolewa na
wafadhili kwa ajili ya kupambana na malaria zinatumika kwa matangazo
ambayo mengi hayana tija.
Waziri amemwagiza Katibu Mkuu kushughulikia matatizo na mapungufu katika
vyuo vya wauguzi ili viweze kutoa watu wenye ujuzi wa hali ya juu
katika kuwahudumia Watanzania.
WATANZANIA 900,000 WANATUMIA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA UKIMWI
Reviewed by Unknown
on
Desemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni: