MBUNGE JAMES MBATIA AVUNJIKA MKONO BAADA YA KUANGUKA...ALAZWA KCMC
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia |
Mbunge
wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amelazwa katika Hospitali ya Rufaa
ya KCMC mjini Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kuvunjika mkono.
Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), amevunjika mkono wa kushoto baada ya kuteleza na kuanguka na
amelazwa katika wodi za watu mashuhuri (VIP).
Msaidizi wa mbunge huyo, Hamis Hamis amesema leo Jumatano Desemba
20,2017 kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 2:45 usiku wakati akiondoka
hotelini kurejea nyumbani.
Hamis amesema Mbatia alikuwa akishuka ngazi katika hoteli ya Uhuru iliyopo eneo la Shanty Town ndipo alipoteleza na kuanguka.
“Bahati nzuri pale kulikuwa na daktari wa KCMC anaiwa Ansbert Sweetbert
ndiye alitoa huduma ya kwanza hadi kumpeleka KCMC,” amesema.
Amesema, “Kwa kweli huyo daktari alikuwa msaada mkubwa. Ndiye
aliyempeleka KCMC na alikaa naye hadi saa nane usiku. Wauguzi na
madaktari KCMC walimpa msaada mkubwa.”
Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alipotafutwa leo mchana
amesema bado maumivu aliyonayo ni makali kutokana na kuvunjika mkono.
“Bado nina maumivu makali. Nashukuru sana Mungu na jopo la madaktari limeshakutana na watafanya uamuzi,” amesema.
Mbatia amesema alishapatiwa matibabu ya mwanzo baada ya vipimo vya X-Ray
kuthibitisha amevunjika mkono, lakini madaktari wanafanya tathmini ni
huduma gani zaidi apewe.
MBUNGE JAMES MBATIA AVUNJIKA MKONO BAADA YA KUANGUKA...ALAZWA KCMC
Reviewed by Unknown
on
Desemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni: