Uganda yaondoa kikomo cha umri wa kugombea urais
Wabunge wa Uganda wameyapitisha
mabadiliko ya Katiba ambayo sasa yanamruhusu Rais wa sasa Yoweri Kaguta
Museveni kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa kwa muhula wa sita.
Wabunge wa upinzani walitoka ndani ya ukumbi zaidi ya mara moja na sita kati yao walifukuzwa ukumbini kutokana na kuupinga muswada. Na hatimaye spika wa bunge hilo Bi Rebecca Kadaga akitangaza matokeo baada ya kupiga kura ya mwisho ikiwa wapiga kura wawili hawakuwa na upande, upinzani wamepata kura 62 na wanaotaka kuondowa kikomo kura 315 na hivyo Spika kutangaza kuwa mswaada huo umepita baada ya kusomwa mara ya tatu.
Wabunge pia wamerejesha ukomo wa vipindi viwili vya kukaa madarakani kutoka miaka saba hadi miaka mitano, kwa hivyo wabunge wa sasa wataendelea kuongoza hadi mwaka 2023.
Ni pengine kutokanana malalamiko kuwa kuondolewa kwa ukomo wa umri kunaweza kumfanya Bwana Museveni kuwa Rais wa milele. Wafuasi wa Museveni wanadai ni waganda ndiyo wanaweza kumwondoa madarakani kwa Kura.
- Wabunge wapitisha muswada wa ukomo wa umri wa rais Uganda
- Mjadala wasitishwa baada wanajeshi 'kuingia' bungeni Uganda
- Bunge la Uganda lajadili ukomo wa Urais kwa siku ya tatu
Lakini upande wa chama tawala ulitumia kila mbinu kuona kwamba mswaada huo unapita ili Rais Museveni kuendelea kutawala .
Kupitishwa mswaada huo kunampatia tena Rais Museveni kutawala miaka mingine 14 kulingana na mswaada huo, lakini raia wa Uganda wengi walikuwa hawaungi mkono kubadilishwa kwa katiba kumuongeza Rais Museveni kutawala baada ya kutawala zaidi ya miongo mitatu.
Uganda yaondoa kikomo cha umri wa kugombea urais
Reviewed by Unknown
on
Desemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni: