Wabunge wa Tanzania, Burundi Wamkataa Spika wa EALA
Baada
ya Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika mashariki kuchaguliwa na wajumbe
wa nchi nne za jumuiya badala ya sita wabunge kutoka Burundi na
Tanzania na Burundi wamesema uchaguzi huo umekiuka misingi na kanuni za
Jumuiya hiyo.
Wakizungumza
na waandishi wa habari Jijini Arusha, Mwakilishi wa wabunge hao
wamesema hakukuwa na sababu ya kutumia nguvu,jazba na uharaka wa
kumchagua Spika kabla ya hoja zao ikiwemo ya kutaka kupata ufafanuzi wa
mzunguko wa kumpata spika haujatolewa na kwamba hawakubaliani na suala
hilo na endapo hali isipodhibitiwa malengo ya kuundwa kwa jumuiya hiyo
hayatatimia.
Kwa
upande wao Wabunge kutoka Tanzania wamesema hatua ya wabunge wa bunge
hilo kuanza kukiuka viapo vyao muda mfupi baada ya kuapishwa ni dalili
za kukosa moyo wa uvumilivu, umoja, na ushirikiano wa dhati ambao kwa
muda wote ndio umekuwa msingi wa jumuiya hiyo na sio dalili nzuri hasa
ikizingatiwa kuwa miongoni mwa malengo ya jumuya ni kudumisha mshikamano
na kwamba kilichofanyika ni sio kumchagua Spika bali ni maoni yao kuwa
Mh. Martin anafaa kuongoza.
Aidha
Wabunge wa Tanzania wamesema kuwa wanaendelea kuziomba ngazi
zinazohusika kuangalia upya suala hilo na kutoa nafasi ya majadiliano
kwani ndio msingi wa kupata suluhu.
Kufuatia
hali hiyo wabunge kutoka Burundi licha ya kudai kuwa hawamtambui Spika
aliyechaguliwa wamesema hawawezi kushiriki kikao chochote
kitakachoendeshwa na spika huyo.
Wabunge
hao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliapishwa siku ya tarehe 18 /12
/2017 na wakati wa kumchagua spika uliibuka mjadala unaodaiwa
kusababishwa na taarifa zilizotolewa na katibu wa Bunge kuwa wabunge wa
nchi zote ispokuwa uganda wanaweza kuomba kugombea uspika wakati
utaratibu wa awali ulikuwa ni wa kufuata mzunguko.
Wabunge
hao wamefafanua kuwa hata kama mzunguko ungezingatiwa bado lingehitaji
ufafanuzi ambao ungezihusisha Burundi, Rwanda na Sudani Kusini suala
ambalo wanasema licha ya kuliwasilisha lilipuuzwa.
Wabunge wa Tanzania, Burundi Wamkataa Spika wa EALA
Reviewed by Unknown
on
Desemba 20, 2017
Rating:
Hakuna maoni: