HABARI MBILI ZA MAGAZETI YA LEO
1: HABARI LEO Jaji Mkuu: Kushinda, kushindwa yote ni haki
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema siyo sahihi mtu kufi kiri ili vyombo vya sheria hususani Mahakama ionekane imetenda haki, lazima ashinde kesi.
Amesema, msingi bora wa haki ni pamoja na wahusika kupata suluhu nje ya mahakama. Jaji Mkuu Juma alisema hayo jana wakati akifungua Wiki ya Utoaji wa Elimu ya Sheria katika maadhimisho yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kilele cha Maadhimisho haya kitafanyika Februari 1, 2018 kikiongozwa na Rais John Magufuli katika Viwanja vya Mahakama vilivyopo Mtaa wa Chimala, Dar es Salaam. Kaulimbiu ya mwaka huu ni, “Matumizi ya Tehama Katika Utoaji wa Haki kwa Wakati na kwa Kuzingatia Maadili.”
Ufunguzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sheria wakiwamo majaji, wasajili wa mahakama, mahakimu, mawakili na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria. “Mahakamani siyo lazima ushinde…
HABARI LEO :
USIMAMIZI mzuri na utekelezaji wa sera mbalimbali za kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kujenga na kumiliki uchumi, kumeifanya Tanzania kuibuka kinara miongoni mwa nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na Uchumi Jumuishi unaokua duniani.
Taarifa iliyotolewa na Word Economic Forum (WEF) kupitia mradi wake wa ‘The Inclusive Development Index’, imeitaja Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na ya 48 kati ya nchi 103 zilizofanyiwa tathmini ya nchi zenye Uchumi Jumuishi duniani.
Katika orodha ya nchi 10 bora, nchi zilizofuatia za Afrika na nafasi ziliyoshika kidunia ni Ghana (52), Cameron (53), Burundi (55), Namibia (56), Rwanda (57), Uganda (59), Mali (60), Senegal (61) na Nigeria (63).
Takwimu za ukuaji huu zinaakisi moja kwa moja kauli ya Rais John Magufuli ambaye amekuwa akielezea kutaka uchumi wa Tanzania umilikiwe na wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo kutekeleza sera ya uchumi wa viwanda ambao Watanzania wengi hivi sasa wamekuwa wakitekeleza sera hiyo kwa kuanzisha viwanda vikubwa na vidogo

Uchumi Tanzania wagusa wananchi

Reviewed by Unknown
on
Januari 29, 2018
Rating:
Hakuna maoni: