WABUNGE TANZANIA WATAKIWA KUWASILISHA TAARIFA ZAO ZA MIAMALA YA BENKI
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewaandikia barua baadhi ya
wabunge, ikiwataka kuwasilisha taarifa za miamala ya benki za kuanzia
Januari hadi Desemba 2017.
Sekretarieti hiyo imetaka taarifa hizo ziwe zimeifikia ndani ya siku 30 kuanzia Januari 15, 2018.
Barua hiyo inawataka wabunge hao kutekeleza agizo hilo ili kuthibitisha taarifa zilizomo kwenye tamko lake alilowasilisha.
Ofisa mmoja wa taasisi hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe,
alithibitisha kuwepo kwa barua hizo, akisema si wote walioandikiwa barua
za kutakiwa kutoa taarifa hizo.
Hata hivyo, alisema wabunge walioandikiwa ni wale ambao fomu zao zinaonyesha haja ya uhakiki zaidi wa taarifa zao.
Rais wa John Pombe Magufuli ndiye alikuwa wa kwanza kuwasilisha fomu
yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala
Jijini Dar es Salaam Desemba 28, 2017.
Baada ya kuwasilisha fomu hiyo, Rais aliipongeza sekretarieti hiyo kwa
kazi inazofanya na kumtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu, Harold
Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye angeshindwa kuwasilisha
tamko la kabla ya Desemba31, 2017.
Kauli hiyo ya Rais iliwaamsha viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge na
viongozi wengine wa Serikali kufurika kwenye ofisi hiyo kuwasilisha
matamko yao ya mali walizonazo.
WABUNGE TANZANIA WATAKIWA KUWASILISHA TAARIFA ZAO ZA MIAMALA YA BENKI
Reviewed by Unknown
on
Januari 20, 2018
Rating:
Hakuna maoni: