Waziri wa Kikwete arudi CCM atwae jimbo 2020
Mwanasiasa
wa upinzani na aliyekuwa Naibu Waziri katika serikali ya Rais mstaafu
Jakaya Kikwete, Goodluck Ole Medeye, ametangaza kurejea Chama Cha
Mapinduzi huku akidai kuwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa vitendo vya
rushwa,-Hususan nyakati za uchaguzi, vimemalizwa na Mwenyekiti wa chama
hicho, Dk. John Magufuli.
Ole
Medeye juzi alisema kilichomkimbiza CCM mwaka 2015 na kujiunga na
Chadema ni vitendo vya rushwa katika mchakato wa kupata wagombea wa
chama hicho tawala.
Alisema
anafurahi kuona sasa vitendo hivyo havipo ndani ya CCM baada ya
kudhibitiwa na Rais Magufuli.Ole Medeye alikuwa mmoja wa wabunge watano
wa CCM waliojiunga na Chadema Agosti 12, 2015 wakiongozwa na Waziri Mkuu
wa zamani, Edward Lowassa (Monduli).
Ole
Medeye aliteuliwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge baada ya Uchaguzi Mkuu.
Wengine
waliohama pamoja na Lowassa ni Makongoro Mahanga (Segerea), James
Lembeli (Kahama) na mbunge wa viti maalum, Esther Bulaya ambaye sasa ni
mwakilishi wa wananchi wa Bunda Mjini (Chadema).
Hata hivyo, Ole Medeye alihama Chadema kabla ya mwaka kumalizika na kujiunga na UDP kinachoongozwa na John Cheyo Juni 12, 2016.
Medeye
alisema alihamia UDP kwa kuwa inasimamia haki na demokrasia na kwamba
yeye alikuwa akitaka demokrasia ya kweli na jukwaa la haki katika kuleta
haki na maendeleo kwa Watanzania.
Alisema kuwa alikaa chama hicho cha 'Bwana Mapesa' kwa miezi mitatu tu hata hivyo, kwa kuwa "nilikwenda kufanya kazi maalum."
Na
sasa, Ole Medeye amesema ameamua kurejea CCM kwa kuwa kila mwanachama
anayo fursa kushiriki uchaguzi, ikiwamo kugombea nafasi yoyote bila
kutoa rushwa na akashinda.
"Mimi
sijawahi kuwahonga watu ili wanichague," alisema Ole Mideye na "wakati
huo CCM kulikuwa na rushwa sana; ndiyo maana nikaamua kukimbia.
"Lakini kwa sasa hakuna tena kitu kama hicho, hivyo nimeamua kurejea CCM."
Ole Medeye alisema katika Uchaguzi Mkuu ujao, mwaka 2020, anataka kurudi na kuwatumikia wananchi kupitia nafasi ya ubunge.
Waziri wa Kikwete arudi CCM atwae jimbo 2020
Reviewed by Unknown
on
Januari 20, 2018
Rating:
Hakuna maoni: