Waziri Ndalichako: Atoa wiki moja lasivyo mkataba na TBA utavunjwa.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amechukizwa
na hali ya ujenzi katika Hosteli za Chuo Kikuu cha Taaluma na Tiba cha
Mloganzila na kuipatia wiki moja Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA)
kuhakikisha inarekebisha mapungufu yote.
Profesa
Ndalichako ameyasema hayo leo Jumamosi wakati wa ziara ya kukagua hali
ya ujenzi Mloganzila, ambapo alishuhudia ujenzi huo ukiwa umesimama
huku kukiwa na uchimbaji wa msingi pekee katika majengo manne.
Amesema
hajaridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo, licha ya yeye kutoa kiasi cha
Sh3.9 bilioni Agosti mwaka jana kwa ajili ya ujenzi huo wa majengo saba
ambayo yangehusisha mabweni mawili ya wanafunzi, jengo la kufundishia,
jengo la maktaba, bwalo la chakula, jengo la maabara, jengo la maabara
maalum na jengo la kazi za nje.
"Hamko
makini na kazi yenu, niwahakikishie ikifika Jumamosi sijaona
kinachoendelea nawachukulia hatua haiwezekani nimewapa fedha tangu
Agosti mwaka jana mpaka leo mmenichimbia msingi pekee, nahangaika ujenzi
ukamilike madaktari wakae hapa watoe huduma kwa wagonjwa ninyi mnaleta
mchezo, nipo kazini lazima mtii ninachokiagiza," aling'aka Profesa
Ndalichako.
Meneja
wa TBA Kanda ya Dar es Salaam, Manasseh Shekalaghe amesema
kilichokwamisha ujenzi huo ni mvua zilizonyesha ambazo zilileta
changamoto na hivyo msingi ulifukiwa na udongo.
Waziri Ndalichako: Atoa wiki moja lasivyo mkataba na TBA utavunjwa.
Reviewed by Unknown
on
Januari 20, 2018
Rating:
Hakuna maoni: