Jaji Mkuu Aionya Serikali
Jaji
Mkuu nchini Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa
kufanya maamuzi kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika
kukabiliana na upinzani.
Jaji
Maraga ametoa kauli hiyo ikiwa imepita masaa kadhaa tokea kufukuzwa kwa
mwanasheria maarufu ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia
kuapishwa Raila Odinga katika uwanja wa ‘Uhuru Park’ kufukuzwa nchini
humo na kupelekwa Canada.
Katika
ukurasa wake wa Twitter Jaji Maraga amesema malalamiko yaliyopelekwa
Mahakamani yalikuwa wazi na majukumu ya kufanyia maamuzi yalikuwa ya
Mahakama kutokana na kwamba ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila
mmoja pamoja na serikali yenyewe.
Jaji
huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria
kutokana na kitendo cha serikali ya Kenya kuonekana kudharau maamuzi ya
mahakama
Jaji Mkuu Aionya Serikali
Reviewed by Unknown
on
Februari 08, 2018
Rating:
Hakuna maoni: