Majibu ya Serikali Kuhusu Zile Milioni 50 Ilizoahidi Kwa Kila Kijiji
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi
amesema kuwa serikali itaweka utaratibu utakaowezesha kutekelezwa kwa
ahadi ya kutolewa milioni 50 kila kijiji, hivyo wananchi wasiwe na hofu.
Dkt
Abbasi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali na miradi
inayotekelezwa na serikali, na kuweka bayana kwamba, tayari mambo
makubwa zaidi yameshafanyika, na hivyo hilo la milioni 50 kila kijiji
litatekelzwa pia.
Majibu
hayo aliyatoa baada ya mmoja wa waandishi wa habari kuulizwa swali,
baada ya kuona ni mwaka wa tatu sasa tangu Rais Dkt Magufuli alipoingia
madarakani, lakini ahadi yake ya kutoa TZS milioni 50 kila kijiji kwa
ajili ya kuwasaidia kina mama na vijana kujikwamua kiuchumi
haijatekelezwa.
“…
50 nyenyewe tutaweka utaratibu itakuja tu ikifika. Lakini maji si
yanakuja bana, dawa si zipo, barabara si zipo, sasa kama wewe ulitaka
ile 50 ili upige dili, tulia kwanza.”
Aidha,
Dkt Abbasi amesema kwamba, ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) haikusema
ni lini ahadi hiyo itatekelezwa, kama ni 2017 au 2018, hivyo akawataka
wananchi kuwa na subira, pindi utaratibu ukikamilika watapatiwa fedha
hizo.
==>Msikilize hapo chini
==>Msikilize hapo chini
Majibu ya Serikali Kuhusu Zile Milioni 50 Ilizoahidi Kwa Kila Kijiji
Reviewed by Unknown
on
Februari 08, 2018
Rating:
Hakuna maoni: