Waziri Mkuu Majaliwa ahamasisha uliamaji wa mazao matano makuu ya biashara
Serikali inaendelea na mpango wa kuhamasisha ulimaji wa mazao makuu matano ya Pamba, Korosho, Tumbaku, Kahawa na Chai nchini ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo jana Bungeni Mjini Dodoma
wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Sumve Mhe. Richard Ndassa juu ya namna Serikali ilivyojipanga na
utafutaji wa masoko ya Pamba kutokana na mwitikio mkubwa wa kulima zao
hilo mwaka huu.
“Miongoni
mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na
kutafuta masoko ndani na nje ya nchi,” alisema Waziri Mkuu.
Amesema,
mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini
ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya
Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.
Pia,
Mhe. Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Liwale Mhe. Zuberi
Kuchauka juu ugawaji wa pembejeo za korosho kwa mwaka huu alisema,
Serikali ilitoa pembejeo ya Salfa bure mwaka jana kwa wakulima wa
korosho ili kufanya hamasa kwa zao hilo baada ya wakulima kutelekeza zao
hilo kutokana na kukosa pembejeo hiyo.
“Baada
ya ugawaji wa pembejeo hiyo ya Salfa zao hilo limevunwa kwa kiwango cha
juu kwa mwaka jana, hivyo kutokana na fedha walizozipata wakulima wa
zao hilo watatatikiwa kuchangia gharama za Salfa kwa mwaka huu,” alisema
Mhe. Majaliwa.
Wakati
huo huo, Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa
Urambo Mhe. Margaret Sitta juu ya migogoro ya mipaka ya mapori na
misitu, alisema Serikali imeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii
kushirikisha wanavijiji na viongozi wa kijiji wakati wa uwekaji wa
mipaka hiyo.
Hata
hivyo alisema ikiwa kijiji kitaonekana kiko ndani ya mipaka ya msitu au
pori, tathmini itafanyike na baadae watapewa elimu ya kutoingia ndani
ya mipaka ya misitu na mapori ya Serikali Kuu
Misitu yote ya Serikali Kuu inahifadhiwa kisheria na mipaka hiyo inaonekana ili kuondoa migogoro na wananchi.
Waziri Mkuu Majaliwa ahamasisha uliamaji wa mazao matano makuu ya biashara
Reviewed by Unknown
on
Februari 08, 2018
Rating:
Hakuna maoni: