Serikali yatenga fedha kumaliza migogoro sugu ya ardhi kwenye maeneo ya jeshi
Na Regina Mkonde
Serikali
kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imeahidi kuondoa
migogoro ya ardhi kati ya wananchi na jeshi kwa kulipa fidia wananchi
ambao ardhi zao zimechukuliwa na Jeshi bila kulipwa kwa muda mrefu.
Ahadi
hiyo imetolewa jana Februari 8, 2018 Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi wakati akijibu
swali la Mbunge wa Dimani Juma Ally Juma lililohoji mpango wa serikali
katika kutatua mgogoro wa muda kati ya Jeshi na Wananchi wa eneo la
Kisakasaka, visiwani Zanzibar.
Dkt.
Mwinyi alisema wizara yake imetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka wa
fedha wa 2017/18 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wanaostahili hasa
wale waliochukuliwa maeneo yao na Jeshi pasipo kulipwa fidia.
“Kambi
nyingi ambazo zina migogoro ya ardhi, iko ya aina nyingi kuna migogoro
ambayo Jeshi limechukua ardhi ya wananchi hawajalipa fidia, wananchi
wamevamia maeneo ya kambi na kadhalika, tumeweka fedha kwenye bajeti ya
wizara ili kwenye maeneo ambayo fidia zinahitajika tuweze kulipa fidia,
ili kumaliza migogoro, mwaka wa bajeti haujaisha na ni mategemeo yetu
fedha zikipatikana tuanze kulipa fidia kwa wanaostahili kulipwa fidia
maana wengine wapo wamevamia hawastahili kulipwa fidia,” alisema.
Kuhusu
mgogoro wa Kisakasaka, alisema serikali inautambua mgogoro huo
uliokuwepo tangu mwaka 1979, na kwamba kilichokwamisha utatuzi wa
mgogoro huo ni ukosefu fedha jambo ambalo wizara yake imetenga fedha ili
kuleta suluhisho la kudumu kwenye mgogoro huo.
“Wizara
ya ulinzi inatambua uwepo wa mgogoro wa ardhi kati ya jeshi na wananchi
katika eneo la kisakasaka, katika kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro
huu, makao makuu ya jeshi imeridhia kurekebisha mpaka wa kambi ya
kisakasaka ili kuwaachia wananchi eneo la mgogoro na hivyo kuleta
suluhisho la kudumu kwenye mgogoro huo. Zoezi hilo halijafanyika
kutokana na ufinyu wa bajeti, hata hivyo katika mwaka huu wa fedha wa
mwaka 2017/18 tunategemea kutekeleza zoezi hilo,” alisema.
Aidha,
Dkt. Mwinyi amewasihi wananchi wa Kisakasaka kuwa wastahimilivu wakati
serikali inachukua hatua stahiki ili kuzuia madhara yoyote yanayoweza
kutokea, endapo wataendelea na shughuli za kilimo na mifugo katika eneo
hilo.
Serikali yatenga fedha kumaliza migogoro sugu ya ardhi kwenye maeneo ya jeshi
Reviewed by Unknown
on
Februari 08, 2018
Rating:
Hakuna maoni: