Mkuu wa Mkoa,Panya wamkera atoa maagizo kwa viongozi
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya
Sumbwanga Dk. Khalfan Haule kuhakikisha anatafuta dawa ya kuulia panya
wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na uchomaji wa misitu
kwasababu ya uwindaji wa panya.
Amesema
kuwa ameisikia changamoto hiyo ya uchomaji wa misitu kwasababu ya
uwindaji wa panya kutoka kwa vijana mbalimbali wanaojishughulisha na
mashamba ya upandaji miti pamoja na taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga juu ya changamoto za kuendeleza
misitu.
“DC
tafuta dawa ya panya, wauliwe huko mashambani, ili panya wasiwepo na
miti iokoke, mbona hamshangilii? Hawa panya tutawaua kwa sumu huko
mashambani wasiwe chanzo cha mioto ambayo mnachoma huko kuwatafuta hawa
panya ili wafie huko huko mashimoni msiwapate,” alisisitiza.
Agizo
hilo amelitoa katika muendelezo wa kampeni ya upandaji miti mijini na
vijijini katika Kijiji cha Mpwapwa, kata ya Mpwapwa, Wilayani Sumbwanga
baada ya kuwauliza wananchi wa Kijiji hicho juu ya changamoto
aliyoisikia ya uchomaji wa moto misitu kutokana na kuwinda panya, japo
wananchi walikataa.
Pia
katika kuongezea hilo alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga kuhakikisha anasimamia sheria ya hifadhi ya mazingira na
kuwawajibisha wote wanaohusika na uharibifu wa mazingira.
Nae
akisoma taarifa Mkurugenzi wa H/W ya Sumbawanga Nyangi Msemakweli
alibainisha kuwa miongoni mwa changamoto ni muitikio mdogo wa uhifadhi
wa mazingira pamoja na mila na tamaduni za wananchi za uwindaji wa panya
hali inayosababisha uchomaji wa misitu wakati wa kiangazi.
“Changamoto
nyingine ni baadhi ya viongozi wa serikali ya Kijiji kujihusisha na
uuzajia wa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya hifadhi ya Kijiji na
usimamizi mdogo wa sheria ndogo za vijiji katika utunzaji wa misitu,”
Alimalizia.
Mmoja
wa vijana wanaojishughulisha na upandaji kiti wa kibiashara Julius
Magaga alimweleza Mh. Wangabo kuwa chnagmoto inayowakatisha tamaa vijana
wengi ni kutokana na uwindaji wa panya uliokithiri na kusababisha
hasara katika misitu.
Kwa
msimu wa 2017/2018 hadi 30/1/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga
imepanda miti 830,527 ambayo ni sawa na 55.4% na ina misitu 92 yenye
ukubwa wa jumla ya Hekta 49,179.6. Huku Mh. Wangabo akigawa miche 850
kwa kaya 850 za Kijiji cha Mpwapwa, Wilayani Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa,Panya wamkera atoa maagizo kwa viongozi
Reviewed by Unknown
on
Februari 08, 2018
Rating:
Hakuna maoni: