Mapigano kusitishwa Jumamosi Ukraine?
Viongozi wa mataifa ya Ulaya
wamesema kuwa wataiwekea vikwazo zaidi Urusi iwapo itashindwa kusimamia
makubaliano mapya yaliyofikiwa kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine.
Kansela
wa Ujeruman Angela Merkel amesema kuwa tayari mataifa hayo
yalishakubaliana vikwazo hivyo itakavyo wekewa Urusi iwapo itakiuka
makubaliano hayo. Markel aliyasema hayo muda mfupi baada ya viongozi hao
wa Ulaya kuwasilisha makubaliano yanayo zihusisha Ukaraine na Urusi
kufuatia machafuko yanayoendelea. Usitishaji wa mapigano mashariki mwa
Ukraine unatarajiwa kuanza rasmi Jumamosi usiku,hata hivyo wanajeshi wa
Ukraine na Waasi wa Urusi wapo katika hali ya wasiwasi kufuatia
makubaliano hayo mapya huku kila upande ukiangalia mwingine katika
utekelezaji wa kuelekea kuleta Amani mashariki mwa Ukraine.
Mapigano kusitishwa Jumamosi Ukraine?
Reviewed by Unknown
on
Februari 12, 2015
Rating:
Hakuna maoni: