Albert Msando atoa neno Baada ya Kuteuliwa na Rais Magufuli
Mwanasheria Albert Msando amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa miongoni mwa watu 9 ambao watakuwa na jukumu la kufuatilia na kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kote nchini.
Albert Msando ameandika ujumbe huo wa shukrani kwenye ukurasa wake wa instagram, na kusema kwamba anaamini kazi hiyo itafanyika kwa weledi.
“Namshukuru Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uteuzi wa kuwa mjumbe wa Tume ya Kufuatilia Mali za Chama. Chini ya uenyekiti wa Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na wajumbe wengine wa tume.Nnaamini kwa dhati kazi hii itafanyika kwa weledi ili kukiwezesha chama cha Mapinduzi kujitegemea kupitia mali zake”, ameandika Albert Msando
Hapo jana Rais Magufuli ameteuwa timu ya watu 9 ambao wataunda tume ya kufuatilia na kuhakiki mali za CCM nchini kote, baada ya kubaini kuna baadhi ya mali haziingizi kipato stahiki.
Albert Msando atoa neno Baada ya Kuteuliwa na Rais Magufuli
Reviewed by Unknown
on
Desemba 21, 2017
Rating:
Hakuna maoni: