NSSF KUWACHUKULIA ATUA KALI WAAJIRI MKOANI TANGA
Baadhi ya waajiri mkoani
TANGA,wanatarajiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutowasilisha michango
ya makato ya kila mwezi ya wafanyakazi wao katika shirika la taifa la hifadhi
ya jamii NSSF.
Akizungumza na MBONIYETU leo,meneja
wa NSSF mkoa wa Tanga Ndugu.ELINAMI MASAOE,amesema hatua hiyo inajiri kutokana
na mkoa huu kuwa na idadi kubwa ya waajiri wanaokihuka sheria na taratibu za shirika
hilo ambapo ni wagumu kuiwasilisha michango ya wafanyakazi wao.
Amesema kwa kipindi
kilichopita walikua na kesi kumi na nne mahakamani ambapo kesi saba walishinda na
zengine saba bado zinaendelea kusikilizwa na kesi zote zinawahusu waajiri wanaokihuka
sheria za shirika hilo.
Aidha amesema wanakutana na changamoto
nyingi ikiwemo ya baadhi ya wanachama wa shirika hilo kugushi nyaraka kwa lengo
la kuweza kupatiwa mafao yao ambapo ametoa rai kwa wanachama hao kuacha mara
moja mchezo huo kwani ni kosa kisheria na kusema wapo mbioni kufuatilia kwa
karibu makato ya wafanyakazi wanayokatwa na waajiri wao kila mwezi,kuongeza
mafunzo kwa waajiri na wanachama wa shirika hilo ili watambua juu ya dhana zima
ya mifuko ya shirika hilo.
NSSF KUWACHUKULIA ATUA KALI WAAJIRI MKOANI TANGA
Reviewed by Unknown
on
Desemba 21, 2017
Rating:
Hakuna maoni: