Wanyarwanda kurudishwa
Mataifa
mbalimbali duniani, hayatawatambua tena raia wa Rwanda waliokimbia nchi
yao kati ya mwaka 1959 hadi 1988 kama wakimbizi baada ya muda waliopewa
kurudi nyumbani kumalizika mwisho wa mwaka 2017.
Hatua
hiyo inaamanisha kuwa, raia hao wa Rwanda hawatatambuliwa kama
wakimbizi na hawatapa msaada wowote kutoka kwa Shirika la Umoja wa
Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR.
Disemba
31 mwaka jana, ilikubaliwa kati ya serikali ya Rwanda na Shirika la
UNHCR pamoja na mataifa mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwapa hifadhi
wakimbizi hao kutoka Rwanda warejee nyumbani.
Mkataba
wa kurejesha nyumbani wa wakimbizi uliokubaliwa mwaka 1951, unawataka
wakimbizi kurejea katika nchi zao baada ya kubainika kuwa, hawapo tena
katika hatari ya kushambuliwa au kunyanyaswa.
Wanyarwanda
wanaoishi nje ya nchi yao ambao wamekuwa wakifahamika kama wakimbizi ni
takriban elfu 20 kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
Wanyarwanda kurudishwa
Reviewed by Unknown
on
Januari 02, 2018
Rating:
Hakuna maoni: